×

Rais Samia Mgeni Rasmi Katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia leo – Video

Rais Samia akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Group Six Bw. Janson Huang kuhusiana na Uwekezaji ambao Kampuni hiyo imefanya wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.

Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Zambia Oktoba 23, 2023 kuanza ziara ya kitaifa ya siku tatu nchini humo.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Rais Samia alilakiwa na mwenyeji wake, Rais Hakainde Hichilema na viongozi wengine wa taifa hilo.

LEO, Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia na keshokutwa anatarajiwa kuwa Rais wa kwanza wa Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita kuhutubia Bunge la Zambia

Rais Samia akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa PMM Group Dkt. Judith Mhina Spendi kuhusiana na masuala mbalimbali ya Kibiashara wakati akielekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais  Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa PMM Group Dkt. Judith Mhina Spendi kuhusiana na Mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali anazokutana nazo katika Biashara wakati akielekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais Samia akimsikiliza Mwenyekiti wa State Oil Group Bw. Nilesh Suchak kuhusu changamoto mbalimbali katika Biashara ya Mafuta wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais Samia akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Bw. Elias Lukumay kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo pamoja na Mafanikio katika Sekta ya usafirishaji wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)

Leave a Comment