Mtangazaji wa Kipindi cha Mapito kinachorushwa na @255globalradio na Global TV, @zali_mapito ametwaa tuzo ya Young CEO’s Africa, katika kipengele cha Social Activism Organisation kupitia Taasisi ya Mapito Foundation Africa.
Zali alikabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, @napennauye huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo na watu wengine mashuhuri.