×

LATRA Yatangaza Ongezeko La Nauli Kwa Mabasi Ya Mjini Na Mabasi

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za Masafa Marefu na Masafa Mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini

Kwa mujibu wa #LATRA nauli za safari zisizozidi Kilometa 10 ambazo zilikuwa Tsh. 500 sasa itakuwa Tsh. 600. Kwa safari za Kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa Tsh. 550 sasa itakuwa Tsh 700

Kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa Tsh. 600 sasa itakuwa Tsh. 800 huku kwa safari za Kilometa 21 hadi 25 nauli imepanda kutoka Tsh. 700 hadi Tsh. 900. Kilometa 26 hadi 30 Tsh. 1100, Kilometa 31 hadi 35 ni Tsh. 1300 na Kilometa 36 hadi 40 Tsh. 1400

Aidha, nauli za Wanafunzi zitaendelea kuwa Tsh. 200 kwa Safari za Masafa Mafupi (Daladala)

 

View this post on Instagram

 

A post shared by LATRA TANZANIA (@latra_tz)

Leave a Comment