
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), leo Desemba 1, 2023 imetembelea Ofisi za Global TV zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam na kufanya semina fupi na viongozi na wafanyakazi wa kituo hicho.
Katika semina hiyo, TCRA imewakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa kuzingatia sheria katika kati ya kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii, kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.
Kwa upande wao, Global TV pia wamewasilisha mapendekezo mbalimbali kwa kamati hiyo kwa lengo la kuboresha uhusiano mzuri kati ya vyombo vya habari na kamati hiyo.
Timu ya TCRA imewajumuisha Saida Muki, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Isaac Mruma na Jackob Tesha ambao ni wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Gloria Rwakibarila na Joseline Ndenje kutoka Sekretariet ya TCRA.