MAHAKAMA ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.
Hati hiyo imetolewa baada ya Zuma kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka kuhusu rushwa yanayo mkabili.
Hati hiyo itafanya kazi mara moja ikiwa Zuma atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza kusikilizwa mwezi Mei mwaka huu.
Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990.
