Mtoto Johnson Noel, amezaliwa akiwa na ulemavu lakini licha ya changamoto hiyo na umri wake mdogo, Mungu amemjaalia upeo mkubwa wa kiakili ambapo anaeleza kwamba ndoto zake ni kuja kuwa rais wa nchi.
Maisha anayoishi Johnson na wazazi wake ni magumu kutokana na hali ya umaskini huku akikosa huduma za kitabibu ikiwemo kufanyishwa mazoezi.
Kipindi cha Mapito kinataka kurudisha tabasamu kwenye uso wa Johnson kwa kuhakikisha anapata sehemu nzuri ya kuishi na wazazi wake na anapata fursa ya kupata elimu.