
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka madaktari na wataalamu wa mifugo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo shughuli za sekta ya mifugo na kuondoa uholela uliopo kwenye sekta mbalimbali.
Amezitaja sekta zenye uholela kuwa ni pamoja na uzalishaji wa vifaranga vya kuku, vyakula vya mifugo, viwanda bubu vya kutengeneza vitotoleshi, uwepo wa dawa bandia sokoni na utumiaji wa dawa za antibiotiki kwa mifugo bila kuzingatia maelekezo ya kitaalamu.

Waziri Ulega ameyasema hayo katika Kongamano la 18 la Chama cha Madaktari Wasaidizi wa Afya ya Mifugo (TAVEPA) unaofanyika jijini Arusha Desemba 12, 2023.
Kufuatia kuwepo kwa shughuli hizo, Waziri Ulega amewataka madaktari na Wataalamu hao wa mifugo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha wanasimamia shughuli zote za sekta ya mifugo zinaendeshwa kwa taratibu zinazoratibiwa vizuri.