
Serikali imeridhia mapendekezo ya timu ya wataalam walioteuliwa kufuatilia mienendo ya mashirika manne, ambapo mashirika manne yamefutwa huku mengine 16 yakiunganishwa.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo imeyataja mashirika yaliyofutwa kuwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPFCS), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Shirika la Elimu Kibaha (KEC) na Bodi ya Pareto.

