
Taarifa ya Ofisi ya Mipango na Uwekezaji imefafanua kuwa hakuna Mtumishi atakayepoteza ajira katika hatua za kuunganisha na kufuta baadhi ya Mashirika ya Umma na Maslahi yao katika Mashirika na Taasisi husika yatalindwa na kuzingatiwa kikamilifu kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma
Taarifa hiyo imetoa zingatio kuwa “Katika Mashirika na Taasisi nyingi za Umma na Serikali kwa ujumla kuna upungufu mkubwa wa Watumishi wa Umma hivyo Watumishi wote ambao Mashirika na Taasisi zao zinaguswa na zoezi hili watapangiwa kazi nyingine katika Utumishi wa Umma na maslahi yao yatazingatiwa ipasavyo.
Taarifa imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo imeyataja mashirika yaliyofutwa kuwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPFCS), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Shirika la Elimu Kibaha (KEC) na Bodi ya Pareto.
