×

Wadau Wa Filamu Wafundishwa Jinsi Ya Kuonesha Filamu Za Hadharani Na Faida Zake

Mkurugenzi Mtendaji wa Ajabuajabu Visual House, Jesse Mpango.

Dar es Salaam 14 Desemba 2023: Kampuni Ya Ajabuajabu ya hapa nchini na A wall Is A Screen ya nchini Ujerumani wameendesha mafunzo ya kuandaa na kuonesha filamu za hadharani pamoja na faida zake.

Mafunzo hayo yamefanyika Alhamisi iliyopita kwenye Ukumbi wa Taasisi ya Kijerumani ya Goethe Institut iliyopo Upanga jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa Ajabuajabu Visual House, Jesse Mpango taasisi hiyo kazi yake kubwa ni kuonesha filamu na kutoa mafunzo kwa mbinu mbalimbali kupitia filamu.

Muongozaji filamu kutoka nchini Ujerumani ambaye ni miongoni mwa wakufunzi hao.

Jesse amesema kazi yao kubwa ni kujenga ufahamu kupitia sinema ili watu waweze kuchagua na kufanya maamuzi ya kuchagua zile filamu ambazo zinagusa vile vitu ambavyo vinawagusa zaidi.

Kitu kikubwa katika mpango huu Jesse amesema ni uratibu wa filamu ambapo sasa hivi wanashirikiana na A Wall Is Screen kutoka Ujerumani ambao wamekuja hapa nchini na kushirikiana na Goethe Insitut kutoa mafunzo ya jinsi ya kuratibu sinema kwenye maeneo ya umma hususan kutumia kuta kama sinema.

Wakufunzi kutoka A Wall Is A Screen wakiendesha mafunzo hayo (washiriki hawapo pichani).

Hii program amesema si mara ya kwanza kufanyika ilianza tangu 2003 ila kwa Afrika hii ndiyo mara ya kwanza inafika hapa Dar es Salaam hii ndiyo mara ya kwanza inafanywa na A Wall Is Screen. Jesse aliongeza kusema;

“Mafunzo haya yatakuwa ya siku mbili leo na kesho, tukiwa na wanafunzi kama 30 hivi ambao watakuwa wanajifunza mbinu za kuchagua filamu, kuendesha mazungumzo na kujenga ufahamu zaidi kwa kitu ambacho wanakionesha mbele za watu na kuchagua maeneo yanayofaa kuoneshea filamu hizo.

Mafunzo yakiendelea.

“Tunashukuru sana ushirikiano mkubwa tuliopewa na Bodi ya Filamu nchini, Goethe Institut na wadau wengine waliotusapoti kwenye mpango wetu huu”. Alimaliza kusema Jesse.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Bodi ya Filamu Tanzania, Ally Makata ambaye alimuwakilisha Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dk. Kiagho Kilonzo amesema mara nyingi Bodi ya Filamu wanaratibu eneo la mafunzo kwa wadau wa filamu na hivyo wao walifika kwenye mafunzo hayo baada ya kualikwa na Ajabuajabu Visual House, Goethe Insitut na A Wall Is A Screen ya Ujerumani.

Afisa Maendeleo wa Bodi ya Filamu Tanzania, Ally Makata.

Afisa huyo amesema lengo mafunzo hayo kwa wadau wetu wa filamu ni kuweza kufahamu kwamba si lazima uwe na mtaji wa milioni 5, milioni 10, wala 20 ili uweze kuandaa tamasha, kumbe yawezekana ukawa na projekta, spika na ukatafuta eneo na ukaweza kuonesha filamu yako ili ufikishe ujumbe uliokusudia kwa jamii.

Afisa huyo amesema kikubwa ni kuanza jambo kabla ya kupata faida kwanza, ukilianza jambo na wengine wakiliona lina manufaa tayari utakuwa umefanikisha lengo. Alimaliza kusema afisa huyo.   HABARI.PICHA NA RICHARD BUKOS GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment