
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo ameteuliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa muda wa miaka mitatu
JamiiForums imekuwa mstari wa mbele katika kupigania uwepo wa Sheria na Kanuni za kulinda faragha na taarifa za watu ili kuwezesha uwepo mazingira rafiki ya matumizi ya dijitali
Wengine walioteuliwa kwenye Bodi hiyo ni Ramadhan Athumani Mungi (Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi) Edward Samweli Lyimo (Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya NBC), Hamid Haji Machano (Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar) na Frida Peter Mwera (Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)