Watu wawili wamefariki (mtoto wa miezi sita na mama mtu mzima) na wengine takribani hamsini wamejeruhiwa katika ajali ya gari basi dogo aina ya Tata liliokuwa linatoka Kigogo Freshi kuelekea Mloka kupitia Kisarawe baada ya kupinduka na kuingia kwenye Mto.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar kunenge alipofika hospitali ya wilaya ya kisarawe kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi hao usiku wa jumatatu Desemba 18, 2023.
Akithibitisha kupokea majeruhi na miili ya waliofariki Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt. Risasi Rajabu amesema baadhi ya majeruhi waliopata majeraha madogo wamesha waruhusu na wengine wanaendelea kuwapatia huduma na wengine saba wamewapatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa Muhimbili.