×

KITIMTIM: Wananchi Watinga Kumng’oa Mwenyekiti Ofisini! – VIDEO

Wananchi wa Kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga Wilayani Chato mkoani Geita wamemkataa mwenyekiti wao, Slivester Nalomba, kwa madai ya kutosomewa mapato na matumizi ya Kijiji pamoja na kushindwa kuanzisha miradi ya maendeleo ya kijiji hicho.

kutokana na hali wanakijiji hao waliamua kumteua mwenyekiti mwingine ili aweze kuwaongoza lakini aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho amegoma kuachia ofisi hiyo huku akiendelea kufanya kazi japo wananchi hawamtaki.