Droo ya tisa ya Kampeni ya Maokoto Chini ya Kizibo inayoendeshwa na Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) imefanyika ambapo jumla ya washindi nane wametangazwa, ambapo kila mmoja amejishindia fedha taslimu, shilingi laki tano (500,000).
Washindi waliotangazwa ni Leonard Kimaya kutoka Gongolamboto, Elizabeth Yaledi kutoka Mbagala na Sostenes Masawe kutoka Goba jijini Dar es Salaam.
Wengine ni Selestine Donat kutoka Arusha, David Pascal kutoka Ifunda, Iringa, Anastoria Robert kutoka Bukoba, Kagera, Maselina Sekela kutoka Mwanza na Stellah Stephan kutoka Dodoma.