×

Joyce Kiria wadau wamjia juu, wamtusi

11659258_498844603624571_214031101422271051_n1Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa hewani kupitia EATV, Joyce Kiria.

Hamida hassan
Katika siku za hivi karibuni, Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa hewani kupitia EATV, Joyce Kiria aliposti picha mbili mtandaoni zikimuonesha ‘robo’ mtupu, jambo lililowafanya baadhi ya wadau wake kumjia juu sambamba na kumtukana.

Picha moja ilimuonesha akiwa amevalia sketi yenye mpasuko mrefu na nyingine akiwa amekaa chini staili ya kukunja nne kisha kuacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake.
Picha hizo zilichafua hali ya hewa mtandaoni kwa watu kumchana kuwa, kwa vile ni mmoja wa wanaotetea haki za wanawake hastahili kuvaa mavazi hayo.

Kufuatia maneno hayo makali na matusi juu, Ijumaa lilimtafuta Joyce aliyefunguka:
“Sivai kumfurahisha mtu yeyote wala sifanyi maisha yangu kuifurahisha jamii, waniache na maisha yangu.

2 Comments

Leave a Comment