Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema kwamba hayuko tayari kubariki ndoa ya jinsia moja kwa sababu ni kinyume na maagano ya Mungu ya kutaka binadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi ulimwenguni.
Askofu Kassala amesema kuwa ni bora abariki jiwe ukajengee nyumba sio kubariki watu wa jinsia moja wanaotaka kufunga ndoa ndani ya kanisa hilo.
Akihubiri katika misa ya kitaifa ya Krisimasi, amesema kubariki mapenzi ya jinsia moja ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka wanadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi.
Amesema binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka na kanisa liyabariki jambo ambalo amelipinga vikali.
“Binadamu amemuacha Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa. Binadamu ameukataa uumbaji na kuendeleza uumbaji na sasa wanafanya mambo machafu yanayomchukiza Mungu, wamekuwa wakiharibu vizazi kwa kutoa mimba na sasa wanataka tubariki na mapenzi ya jinsia moja. Kwangu bora nibariki jiwe lakini sio uchafu huo,” amesema Askofu Kassala.