Mfanyabiashara maarufu nchini, Lilian Mmari @lilian_mmari amefunguka mapito mazito aliyoyapitia kutokana na marafiki ambao alikuwa akila nao pamoja na kufanya naye vitu vingi ambao wamemsababishia matatizo makubwa kwenye familia yake na vitu vingi kuharibika kwenye maisha yake.
Akizungumza na Global TV Online kwa nia ya kutoa mafunzo watu wawe makini na marafiki ambao wanawazunguka kwani ndiyo hao wanaharibu na kuvunja kila kitu kwenye maisha yako.