
Mmiliki wa Baa ya Kitambaa Cheupe iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, Jesca Kikumbi maarufu kama Jesca Kitambaa Cheupe, amesema kuwa baada ya kupokea taarifa za moto kwenye baa yake, aliwahi kufika eneo la tukio na kupiga simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Fire) lakini walichelewa kufika.
Jesca amesema yeye na wafanyakazi wake hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo na kueleza kuwa atatoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo.