Rais Samia Afika kutoa pole kwa familia ya Marehemu Masauni Yussuf Masauni
Global Publishers March 3, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na familia ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni alipokwenda kuhani kufuatia kifo cha Baba yake Mzee Masauni Yussuf Masauni aliyefariki dunia tarehe 23 Februari, 2024. Rais Samia amekutana na familia hiyo nyumbani kwao Migombani, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Machi 3, 2024 amefika nyumbani kwa Marehemu Mzee Masauni Yussuf Masauni, ambae ni Baba Mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Rais Samia amefika kutoa pole kwa familia katika eneo la Migombani, Zanzibar.
Marehemu Mzee Masauni Yussuf Masauni alifariki Februari 23, 2024 katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Februari 24, 2024 katika makaburi ya Mwanakwerekwe,Zanzibar.
Rais Samia akishiriki dua na familia ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.Baadhi ya Ndugu na Jamaa wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni waliojumuika wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokwenda kuhani kufuatia kifo cha Baba yake Mzee Masauni Yussuf Masauni aliyefariki dunia tarehe 23 Februari, 2024.Rais Samia akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni alipokuwa akitoa shukrani kwa Rais kwa kuwatembelea na kuwafariji.