
Kampuni ya huduma za mtandao wa simu za mkononi ya Tigo Tanzania imewakabidhi zawadi mbalimbali zikiwemo Televisheni tano, simu janja ishirini na pikipiki tano wakulima zaidi ya ishirini kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani wakiwa ni washindi wa Kampeni ya Vuna na Tigo Pesa.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao waliishukuru kampuni ya Tigo kwa kampeni hiyo nzuri yenye ubunifu wa aina yake pamoja na zawadi hizo ambazo zitawasaidia kwenye shughuli zao za kilimo na nyinginezo. Wakulima hao wameahidi kuendelea kutumia huduma za Tigo ili kuendelea kunufaika na kampeni hiyo na nyinginezo.
Akizungumza kwenye hafla ya kugawa zawadi hizo Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha aliwashukuru wakulima hao kwa kutumia huduma za Tigo Pesa ambayo imekuwa ikiwarahisishia kuwafikishia pesa kiurahisi haraka na usalama zaidi na kuwahidi kuiboresha zaidi kwa kuongeza ubunifu zaidi ili iweze kuwafikia wakulima wengi zaidi nchi nzima.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala aliipongeza Tigo kwa ubunifu wao wa huduma hiyo nzuri waliyoitoa kwa wakulima hao na kusema;
“Ni ukweli usiopingika kuwa hata pale kwangu Tandahimba wakulima wengi walipitishiwa malipo yao kwenye huduma hiyo ya Tigo na sijawahi kusikia mtu yeyote akilalamika kucheleweshewa malipo yake na hatujapokea malalamiko kwenye ofisi yetu nyingine yeyote kuhusiana na huduma hii.
“Hivyo nitumie nafasi hii kuwapongeza Tigo kwa huduma yao hii nzuri na tunawaombea wazidi kuifikisha sehemu mbalimbali ili na wengine wazidi kunufaika” Alimaliza kusema Kanali Sawala.