×

Mbunge Shigongo Amlilia Zagalo Wa Nyehunge “Alifanya Kazi Usiku Na Mchana Akijituma”- Video

Mbunge wa jimbo la Buchosa ambalo liko wilayani Sengerema, Erick Shigongo

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Sengerema Marco Zagalo amezikwa jana Mei Mosi, 2024 nyumbani kwake, Nyehunge ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, Eric Shigongo ameshiriki mazishi hayo.

Zagalo ambaye alizaliwa mwaka 1961 enzi za uhai wake ameshiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa chama hicho kwa kushika nafasi mbalimbali za ngazi ya kata pamoja na kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza mbele ya waombolezaji walioshiriki kwenye kuaga mwili wa kada huyo, Shigongo ametoa pole kwa msiba huo mzito ambao umewakuta ndugu, jamaa na marafiki huku akitoa rai kwa waombolezaji kumuombea marehemu ili Mungu amuepushe na adhabu za kaburini na kutenda mema wangali hai.

Leave a Comment