Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali wilayani humo ikiwa ni pamoja na kutembelea mradi wa barabara muhimu ya Jaffo yenye urefu wa mita 500 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Magoti amemtaka Meneja wa TARURA wilayani humo, Godfrey Mbena kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo.