
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma imefanikiwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka wastani wa shilingi milioni hamsini na tano kwa mwezi hadi shilingi milioni miamoja sabini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma Chiruku Chilumba amewaeleza waandishi wa habari mkoani humo kuwa ongezeko hilo limefikiwa katika kipindi cha miezi mitatu toka mwezi January hadi Aprili mwaka huu .
Aidha Chilumba amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili kuongeza zaidi kiwango cha makusanyo akisisitiza kuwa fedha inapoongezeka inawezesha halmashauri kujiendesha vizuri katika kuwahudumia wananchi.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya watumishi wakiwemo wakuu wa Idara wamempogeza mkurugenzi wa huyo kwa kuja mbinu shirikishi katika masuala ya ukusanyaji usimamizi na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato.
Katika bajeti ya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kigoma ya mwaka 2022/23 wastani wa makusanyo kwa mwezi ulikuwa shilingi milioni hamsini na tano kiwango ambacho kimeongezeka zaidi ya mara tatu katika bajeti ya mwaka 2023 /24.