×

Global yawamwagia zawadi wasomaji Kibaha

2.Wakielekezana namna ya kujaza kuponi hiyo iliyopo ndani ya gazeti la Uwazi ili kushiriki katika droo ya Shinda Nyumba.Wanafunzi wa chuo cha uuguzi kilichopo eneo la Kibamba Dar wakisoma Gazeti la Uwazi kabla ya kujaza kuponi zao ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.
3.Mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Uwazi akiingia Kuponi yake katika ndoo maalumu ya kushiriki Bahati nasibu hiyo.Mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Uwazi akiweka kuponi yake katika ndoo maalum ya kushiriki bahati nasibu hiyo.
4 Zoezi likiendelea la kuweka kuponi ndani ya ndoo maalum eneo la Stendi ya Kibamba Dar.
5.Ofisa Masoko wa Golabl,Yohana Mkanda (mwenye fulana nyeupe kulia) akimvisha kofia msomaji wa Gazeti la Uwazi baada ya kukata kuponi yake na kushiriki Bahati nasibu hiyo.Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (mwenye fulana nyeupe kulia) akimvisha kofia mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Uwazi baada ya kukata kuponi yake na kushiriki bahati nasibu hiyo.
6.Kuponi zikiingizwa ndani ya ndoo maalumu ya Bahati nasibu.Kuponi zikiingizwa ndani ya ndoo maalum ya bahati nasibu.
7.Wakazi wa eneo la Kibamba wakijaza kuponi zao na kuzikata ili kushiriki Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.Wakazi wa eneo la Kibamba wakijaza kuponi zao na kuzikata ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
8.Zoezi la kujaza na kukata kuponi ili kushiriki kwa wakazi wa eneo la Kiluvya Dar ili kushiriki Bahati nasibu hiyo likifanika.Zoezi la kujaza na kukata kuponi kushiriki bahati nasibu hiyo kwa wakazi wa eneo la Kiluvya Dar likifanyika.
10.Wakazi wa eneo la Mkoa wa Pwani-Kibaha wakiweka kuponi zao ndani ya ndoo maalum ili kushiriki droo ya puili ya Shinda Nyumba.Wakazi wa eneo la Kibaha-Pwani wakiweka kuponi zao ndani ya ndoo maalum ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.
11.Wakazi wa Kiluvya wapewa zawadi zao za kofia kuotoka kwa Ofisa Masoko wa Global,wakati wakishirikia kujaza kuponi na kutumbukiza ndani ya ndoo maalum ili kushiriki Bahati nasibu.Wakazi wa Kiluvya wapewa zawadi zao za kofia kutoka kwa Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda wakati wakishiriki kujaza kuponi na kutumbukiza ndani ya ndoo maalum.
12.Wakazi wa Kibaha wakichangamkia kununua gazeti kwa uwazi ili kuweza kushiriki Bahati nasibu ya shinda nyumba.Wakazi wa Kibaha-Pwani wakichangamkia kununua Gazeti la Uwazi ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
13.Mwanamama(kushoto) akielekezwa namana ya kukata kuponi iliyokatika Gazeti la Uwazi ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.Anayemwelekeza ni Ofisa Usambazaji wa Global,Jimmy Haroub.Mwanamama wa Mkoa wa Pwani (kushoto) akielekezwa namna ya kukata kuponi iliyokatika Gazeti la Uwazi ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.Anayemwelekeza ni Ofisa Usambazaji wa Global,Jimmy Haroub.
14.Mafundi Gereji wa Kibaha nao wakionekana kuchangamkia kununua gazeti ili kuweza kushirki droo ya pili ya Shinda Nyumba.Mafundi Gereji wa Kibaha nao wakionekana kuchangamkia kununua gazeti hilo ili kushirki droo ya pili ya Shinda Nyumba.
15,Ofisa Usambazaji,Jimmy Haroub(kushoto) akimwelekeza msomaji wa Gazeti la Uwazi eneo la Kibaha Stendi namana ya kujaza kuponi yakeOfisa Usambazaji,Jimmy Haroub(kushoto) akimwelekeza msomaji wa Gazeti la Uwazi eneo la Kibaha Stendi namna ya kujaza kuponi yake.
16.Mwanamama akisaidiwa kujaza kuponi yake kutoka kwa Ofisa Masoko wa Global (kushoto),Yohana Mkanda.Mwanamama akisaidiwa kujaza kuponi yake kutoka kwa Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (kushoto).

KAMPUNI ya Global Publishers Ltd,Wachapishaji wa Magazeti yaChampioni,Uwazi,Amani,Risasi,Ijumaa na Ijumaa Wikienda imemwaga zawadi za kofia kwa wasomaji wake, Kibaha-Pwani baada ya kununua Gazeti la Uwazi la jana ili kushiriki droo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Kabla ya kufika katika Mkoa wa Pwani Ofisa Masoko,Yohana Mkanda na Ofisa Usambazaji,Jimmy Haroub walitoa zawadi kwa wakazi wa eneo la Kibamba na Kiluvya zote za jijini Dar waliokutwa wakinunua magazeti ya Uwazi kwa wauzaji wa maeneo hayo ambapo walipata fursa ya kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Zawadi zilizotolewa Mkoani Pwani ni mwendelezo wa zawadi zilizotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Wilaya yake ya Kisarawe ambapo wasomaji walinunua gazeti na kukata kuponi zilizowawezesha kushiriki droo ya pili inayotarajiwa kuchezeshwa hivi karibuni.

Akizungumza na wasomaji wa Mkoa wa Pwani wakati akitoa zawadi hizo,Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda aliwaomba washiriki wajitokeze kwa wingi ili kujinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo kofia, t-shirt pamoja na kumiliki nyumba kubwa na ya kisasa iliyoko eneo la Salasala jijini Dar es Salaam.

“Wananchi wa Mkoa wa Pwani-Kibaha ninawaomba mshiriki kwa wingi ili muweze kujinyakulia zawadi mbalimbali na msomaji mmoja aweze kumiliki nyumba iliyoko eneo la Salasala Dar, kwani hii ni bahati nasibu yeyote anaweza kushiriki,” alisema Mkanda.

Mpaka sasa zawadi zilizokwisha kutolewa kwa wasomaji ni fulana,kofia,simu za kisasa, runinga pamoja na ving’amuzi vya TING huku pia wakiendelea kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya nyumba katika droo ya mwisho.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Leave a Comment