TLS Kusimamia upatikanaji wa sheria na Punguzo la Tozo Asasi za kiraia
Morogoro.Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kupitia kwa kaimu mkurugenzi wake Mackphason Mshana amesema wako kwenye hatua za wa kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa sharia moja itakayoruhusu asasi za kiraia hapa nchini kutimiza majukumu yake bila kuingiliwa

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa TLS Mackphason Mshana akiwa mkoani Morogoro wakati wa mkutano maalum kujadili maoni waliyoyakusanya ambapo amesema kumekuwa na sheria nyingi ambazo zimekuwa kandamizi kwa asasi hizo ambapo katika kurahisisha utendaji wao wa kazi wameamua kuwa na kikao cha pamoja na asasi hizo ili kupata suluhis
“Malalamiko mengi ambayo yanatoka kwa asasi za kiraia ni kuwepo kwa sheria nyingi ambazo zinaangalia sekta ya asasi za kiraia ambapo kuna wakati zinawachanganya ni sheria ipi haswa inapaswa kufuatwa tunachojaribu kukifanya ni kuhakikisha tunakuwa na sharia moja ambayo itaongoza asasi za kiraia

“Pia kumekuwa na malalamiko kutoka kwa asasi za kiraia kwamba pamoja na kwamba asasi hizo zinafanya kazi za kiraia ambazo zilitakiwa kufanywa na serikali lakini bado zinatozwa kodi mbalimbali, kuna tozo ambazo kimsingi zinakubalika lakini changamoto imekuwa kwenye zileshughuli ambazo wanafanya na wanatozwa kodi hilo limekuwa likififisha hizi asasi kufanya shughuli zao na lenyewe tutalitazama na kulifanyia kaz
Suleiman Baitani ni Mratibu wa mtandao wa haki za binadamu Zanzibar THRDC anasema anaamini chama cha wanasheria Tanganyika TLS watafanikisha upatikanaji wa sheria hiyo moja ili kuweka mazingira wezeshi kwa asasi hizo kutimiza majukumu ya

“Mbaya ni kwamba sisi Asasi za kiraia tumekuwa tukifananishwa na wafanya biashara mwisho wa siku tunapata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano asasi haijapata mradi muda mrefu unakuta imeandaliwa malimbikizo ya kodi karibia milioni 300, sisi sio wafanya biashara bali ni watoa huduma maana tunaisaidia serikali pale ambapo haiwezi kutoa hudum” o.i”a”hoa.a huduma”