×

Mamia Wafunguliwa Kimiujiza Kwa Kiboko Ya Wachawi, Simu Zajaa Miamala Ghafla, Wengine Waitwa Kazini

Umati ukifika kanisani kwa Kiboko ya Wachawi Buza Jijini, Dar.

Amini usiamini ushirikina upo na uchawi upo na binaadamu tunafungana saana kiuchawi. Umati mkubwa wa waumini uliofurika kanisani kwa Kiboko ya Wachawi ulionekana kufunguliwa kwenye mapepo yaliyokuwa yakiwawekea vikwazo kwenye kwenye harakati za kimaisha.

Umati ukiwa umeanguka mapepo baada ya kupigwa maombi ya maangamizi ya kuvunjwa nguvu za kichawi.

Katika ibada hiyo umati mkubwa ulionekana kuanguka mapepo na kuombewa na Kiboko ya Wachawi ndipo waliokuwa na shida katika maungo yao walianza kushuhudia uponyaji wa ghafla.

Katika ibada hiyo baada ya muda mfupo wapo walioshuhudia kuingiziwa miamala ya fedha kwenye simu zao kutoka kwa wadeni wao sugu na sehemu nyinginezo huku wengine wakipokea simu za dili nono.

Kiboko ya Wachawi akishusha maombi ya kuvunja nguvu za kichawi.

Wapo walitolewa mapepo siku kadhaa zilizopita ambapo walitoa ushuhuda wa kurudishwa kazini kwa waliosimamishwa, wengine walioomba ajira kuitwa kwenye usaili, wanafunzi nao ndiyo usiseme wapo waliokuwa wakipatwa na usingizi usioeleweka wakati wa kujisomea ambao wameshuhudia kuwa hilo halipo tena. Hizo ni kati ya shuhuda zilizotolewa mbele ya wanahabari wetu kanisani hapo. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL 

Leave a Comment