×

Galatone: Muziki Unatunza Familia Kiaina

Ahmed Sadala ‘Galatone’

Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA AMANI| SHOWBIZ XTRA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Ahmed Sadala ‘Galatone’ amefunguka kuwa pamoja na changamoto nyingi za biashara ya muziki ila bado unamsaidia kiaina kutunza familia yake.

Galatone anayetamba na Wimbo wa Sina Mali na Samaki ameiambia Showbiz Xtra kuwa hali ya biashara ya muziki si nzuri sana lakini angalau anaweza kutunza familia yake.

“Nashukuru si haba, pamoja na ugumu wa soko najitahidi kujichanga hivyohivyo mwenyewe kwa sababu sina meneja na mwisho wa siku napata chochote kwa ajili ya kutunza familia yangu, ambayo ni mama na dada zangu walioko Mkoa wa Tanga,” alisema Galatone.