×

Mapya Yaibuka! Mtuhumiwa Ukatili Wa Watoto Wawili – “Alishawahi Kufanya Tukio Kama Hili Iringa” – Video


Siku kadhaa baada ya mazishi ya mwanamke aliyefariki dunia kutokana na mshtuko alioupata baada ya kugundua kuwa wanaye wawili wamefanyiwa ukatili na mpangaji wao, Global TV kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupinga Ukatili wa Kingono kwa watoto, @bintiwetu.tz imefika nyumbani kwa marehemu.

Foundation ya Binti Wetu imeenda kuwafariji wanafamilia kwa msiba uliotokea na kuangalia namna ya kuwapa msaada wa kisheria ambapo katika mazungumzo na ndugu wa marehemu, mapya yameibuka.

Imeelezwa kwamba mtuhumiwa wa ukatili huo ambaye ametoroka, aliwahi kutuhumiwa kufanya tukio kama hilo mkoani Iringa lakini kesi ikashindwa kuendelea kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kumgia hatiani.

Leave a Comment