
Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wengine kadhaa wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili kaskazini-magharibi mwa Iran.
Helikopta hiyo ilipatikana kaskazini magharibi kwenye mteremko wa kilima katika eneo la Varzaghan, karibu na mpaka wa Azerbaijan Mashariki.
Mapema saa saba hadi nane zilizopita iliripotiwa kuwa ndege hiyo imepata ajali na wataalamu walianza kuisaka mara moja huku hali mbaya ya hewa ikitajwa kama chanzo cha ajali hiyo.
