
Kakika Kuadhimisha miaka 85 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God ni Kanisa lililotokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa AZUSA, California (Marekani), mwanzoni mwa karne iliyopita ya ishirini.
Kanisa la Ubungo Christian Centre Lilifanya Ibada Maalumu ya Jumapili ya Kuazimisha Miaka 85
Ibada Hiyo Iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi Paul Mulokozi Ikiwa ni Kuadhimisha Miaka 85 ya Kanisa la TAG na Miaka 49 ya Kanisa la Ubungo Christian Centre (UCC),

Ambapo Alisema Pamoja na Maadhimisho Kanisa la Limekuwa Likishiliki Katika Shughuli Mbalimbali za Kijamii.
Moja ya Jambo Ambalo Kanisa la Ubungo Limeshiriki Katika Maboresho ya Ofisi ya Serikali za Mtaa Ubungo National Housing na Kuboresha Darasa Katika Shule ya Ubungo National Housing.

Miaka 85 ya uwepo wa Kanisa la TAG inayosherehekewa leo hii, inahesabiwa tangu wakati wa Mmissionari Paul Derr alipolikabidhi Kanisa kwa Baraza Kuu la Assemblies of God Marekani mwaka 1939 na ambao ndio wakati aposimikwa rasmi kuwa mtumishi wa AG na kanisa la Marekani nawala si wakati aipofika Tanganyika akiwa chini ya Kanisa la Pentecoste Holliness Asociation.