×

Simba Yasaka Mbadala wa Mwalimu, Aliyewatungua Yanga Atajwa

Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba SC wapo kwenye hesabu za kusaka mbadala wa Seleman Mwalimu ambaye ametambulishwa katika kikosi cha Yanga SC, Agosti 11,2026 kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.

 

Mchezaji huyo alikuwa kwenye mpango wa Simba SC 2026/27, inatajwa kuwa hawakufikia makubaliano mazuri kwenye upande wa dau jambo lililofanya akakubali kutua Yanga SC, mara baada ya kufikia makubaliano mazuri.

 

Tetesi zinaeleza kuwa Simba SC imeanza mchakato wa kumuulizia kiraka wa Les Aigles du Congo, Tonny Talasi aliyeifunga Yanga SC kwenye mchezo wa Yanga Day, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Agosti 9,2026.

 

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, hivi karibuni aliweka wazi kuwa bado hawajamaliza usajili hivyo mashabiki wawe na Subira.

 

“Usajili bado hatujamaliza  na kuna wachezaji ambao watakuwa kwenye kikosi chetu, kikubwa ni mashabiki kuwa nasi bega kwa bega kila hatua,”

Na Lunyamadzo Mlyuka

 

Leave a Comment