×

Tisa wafariki baada ya jukwaa kuporomoka kwenye mkutano wa hadhara Mexico

Soldiers stand near ambulances after a gust of wind caused a structure to collapse, resulting in multiple fatalities and injuries, at a campaign event for the Citizens’ Movement party, in San Pedro Garza Garcia, Nuevo Leon, Mexico May 22, 2024. REUTERS/Daniel Becerril

Takriban watu tisa wamefariki dunia, akiwemo mtoto, na wengine 50 wamejeruhiwa baada ya jukwaa kuanguka kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la kaskazini la Nuevo León nchini Mexico, gavana wa eneo hilo amesema.

Tukio hilo lilitokea wakati mgombea urais wa mrengo wa kati Jorge Alvarez Maynez alipokuwa akitoa hotuba katika jiji la San Pedro Garza Garcia, karibu na Monterrey.

Bw Maynez hakujeruhiwa katika ajali hiyo, na alionekana akizungumza na wafuasi kufuatia tukio hilo. Washiriki kadhaa wa timu yake walikuwa wamejeruhiwa, alisema.

Kuanguka kulisababishwa na upepo mkali wa ghafla, Bw Maynez alisema kwenye ujumbe wake katika mtandao wa X.

Kanda za video zimeibuka zikionyesha wakati muundo wa taa ulipoporomoka huku watu kadhaa wakiwa jukwaani.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha Bw Maynez akiwapungia mkono wafuasi wake na kisha kukimbilia usalama.

Gavana wa Jimbo hilo Samuel Garcia aliwataka wakazi wa eneo hilo kusalia majumbani kwa sababu ya radi na upepo mkali.

“Ikiwa unaweza, epuka kutoka nje kwa sababu kuna dhoruba na upepo usio wa kawaida. Nitawafahamisha mengi baadaye,” aliandika kwenye mtandao wa X.

Akijibu habari za tukio hilo, Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador alituma salamu za “rambirambi kwa wanafamilia, marafiki wa wahasiriwa na wafuasi wa kisiasa”.

Leave a Comment