×

Wiki Ya Ubunifu, Mabinti Waliopewa Mafunzo Ya Kiteknolojia Na UN WOMEN Waeleza Walivyonufaika

Mratibu wa mafunzo hayo kutoka UN WOMEN, Michael Jerry akizungumza na vyombo vya habari kwenye kongamano hilo.

Dar es Salaam 23 Mei 2024: Wiki ya ubunifu ikiwa inaendelea wasichana kadhaa waliowezeshwa mafunzo ya kidigitali na shirika la Umoja wa Matifa la UN WOMEN wametoa ushuhuda mbele ya wenzao kwenye kongamano lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JICC) jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari Mratibu wa Mipango UN WOMEN Machael Jerry walihusika kutoa mafunzo kwa mabinti hao alisema;

Mmoja wa washiriki akimuuliza swali mnufaika wa mafunzo hayo (hayupo pichani) baada ya kutoa ushuhuda wa alivyonufaishwa.

“Leo hii nafiki mmejionea wenyewe jinsi UN WOMEN kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia Wanawake na Makundi Maalum, tumeweza kuendesha mafunzo ambayo yaliwalenga mabinti wenye miaka 17 mpaka 25.

Mnufaika wa mafunzo hayo akielezea naye alivyonufaika na jinsi atakavyokwenda kuyatumia mafunzo hayo.

“Mafunzo hayo yaliweza kuwawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika teknolojia na masuala mazima ya kidigitali. “Programu hiyo ilianza mwaka jana na iliweza kuwafikia mabinti 110 ambao baadhi yao ndiyo hawa tuliowaona wakitoa ushuhuda na wameweza kusema kwa jinsi gani mafunzo hayo yamewasaidia kuweza kujiajiri au kuajiriwa. Alimaliza kusema Jerry.

Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo aliyejitambulisha kwa jina la Mary Edward amesema analishukuru shirika la UN WOMEN kwa mafunzo hayo ambayo yamewapa uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na masuala ya kiteknolojia.

Leave a Comment