×

Bondwa Hiking Club, Polisi Waipa Moto Kauli ya Waziri Mkuu

Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Morogoro Mhe Latifa Mansoor Mwenye Nguo za Pink akiongoza Mbio zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na Club ya Bondwa Hiking

KLABU ya mazoezi ya Bondwa Hiking ya Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi Mkoani humo limefanya matembezi ya Kms 15 na mbio za Hisani Kms 30 lengo likiwa ni kuunga mkono wito wa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa la kuwata wananchi kushiriki mazoezi ya ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yasio ambukiza.

Mbio hizo ziliongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda Ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor kwa kushirikiana na maafisa askari wa jeshi la Polisi,watumishi wa Mahakama  pamoja na baadhi ya joking club  zilizopo mkoani humo

Aidha katika mbio hizo kuligawanyika kundi jingine ambalo lilotembea umbali wa KM 15 kuzunguka maeneo tofauti ya Ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Morogoro Mhe Latifa Mansoor akimkabidhi cheti cha Pongezi mtoto Ally Seif mwenye umri wa miaka 12 kwa kufanikiwa kumaliza mbio za KM 30
Jaji Mfawidhi Mahakama  Kanda ya Morogoro Mhe Latifa Mansoor Mwenye Nguo za Pink akiongoza Mbio zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na Club ya Bondwa Hiking

Mwenyekiti wa Bondwa Hiking Club Wakili Mwansoho akizungumza mara baada ya matembezi na mbio

Leave a Comment