
Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’ amejiunga na klabu ya Aalborg FC @aabsportdk iliyopanda daraja kwenda Ligi Kuu ya Denmark almaarufu ‘Superliga’ kwa mkataba wa miaka minne.
Kelvin (20) ambaye alikuwa anakipiga kunako klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji yuko nchini Denmark kwa ajili ya kukamilisha usajili huo hali inayopelekea akosekane katika kambi ya timu ya Taifa Stars iliyoko nchini Indonesia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

