Msichana wa mjini ambaye pia ni mtangazaji, Nasra Rajesh ‘Lady Naa’ amepewa ujauzito na mwanamuziki Alawi Junior ambapo inadaiwa kuwa ujauzito huo ni wa miezi sita sasa.
Sosi aliye karibu na mwanamuziki huyo ameliambia Ijumaa kuwa kwa sasa Lady Naa na Juniour penzi ni zito kwani mahaba yamezidishwa baada kubaini kuwa wanatarajia mtoto.
Baada ya ‘ubuyu’ huo kutufikia, Lady Naa alitafutwa na alipopatikana alikiri kuwa na mimba huku akieleza kuwa huenda ndoa ikafungwa baada ya mtoto kuzaliwa.
“Unajua ustadhi amekataa kutufungisha ndoa, anasema si ruhusa kufanya hivyo kwa sababu ya ujauzito, nikishajifungua inshaallah ndoa itafungwa,” alisema Lady Naa.