×

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Atangaza zawadi ya bingwa wa mashindano ya Wazazi Super Cup – Video

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Said Ally.

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Said Ally ametangaza zawadi ya shilingi milioni 5 kwa bingwa wa mashindano ya Wazazi Super Cup Mkoa wa Dar es Salaam.

Mashindano hayo kwa mwaka huu unakuwa ni msimu wake wa pili baada ya kufanyika mwaka jana huku kwa msimu huu zawadi zote zikitarajiwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 20.

Mashindano hayo yanatachezwa kwa kila kata na yanatarajiwa kuanza Juni 8 mpaka Juni 30.

Leave a Comment