×

Waziri Silaa Amwaga Machozi Mgogoro Arusha, Mwananchi Ataka Kunywa Sumu Baada Ya Kuvunjiwa Nyumba – Video

Mkazi wa jijini Arusha ajulikanaye kwa jina la Respis Brasius ambaye amekiri kwamba angekunywa sumu kama asingesikiliza hotuba ya Waziri.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amejikuta akitokwa na machozi wakati akimsikiliza mkazi wa jijini Arusha ajulikanaye kwa jina la Respis Brasius ambaye amekiri kwamba angekunywa sumu kama asingesikiliza hotuba yake ya Bajeti ya Mwaka 2024/2025 wakati akiwasilisha bungeni Dodoma Mei 27, 2024.

Mkazi huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuteseka kwa muda mrefu akitafuta haki yake bila mafanikio kwa kuwa alivunjiwa nyumba yake pamoja na watu wengine katika Mtaa wa Unga Limited jijini Arusha.

Leave a Comment