×

Rais Samia na Rais wa Jamhuri ya Korea Washudia utiaji wa saini wa Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba pamoja na Waziri wa Uvuvi na masuala ya Bahari kutoka Jamhuri ya Korea Kang Do-Hyung wakisaini Hati baina ya nchi mbili kuhusu Ushirikiano katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol wameshudia utiaji wa saini wa Mkataba mmoja, Hati za Makubaliano (MOU) 2 na Tamko la pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi (EPA)

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu ya Jamhuri ya Korea leo Juni 2, 2024.

Rais Samiaakiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakisaini Tamko la Pamoja kuhusu Uanzishwaji wa Majadiliano juu ya Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi.
Shamrashamra za Mapokezi ya Rais Samia atika Ikulu ya Nchi ya Jamhuri ya Korea Jijini Seoul.
Rais Samia akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol.
Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Yoon Suk Yeol kabla ya kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba mbalimbali.
Rais Samia akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nchi hiyo.

MGOGORO MKUBWA wa BABA MCHUNGAJI na WACHUNGAJI WENZAKE – DC AFUNGA KANISA – MAKONDA AIBUA MAZITO…

Leave a Comment