×

FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili Wachezaji

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea klabu ya Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya klabu hiyo kurekebisha upungufu uliojitokeza katika uhamisho wa mchezaji.

Klabu hiyo ilikuwa haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo. Tayari Yanga imeingiza uthibitisho wa malipo hayo katika Mfumo, hatua iliyosababisha ifunguliwe.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imeongezeka kuwa hata hivyo klabu hiyo bado inakabiliwa na adhabu nyingine ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kushindwa kesi ya madai dhidi ya mchezaji Lazarus Kambole raia wa Zambia ambaye alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na kuvunjiwa mkataba.

Leave a Comment