×

Msafara wa Dkt. Nchimbi Wasimamishwa Himo-Moshi

Mamia ya Wananchi wa wamejitokeza kwa wingi kumpokea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel pamoja na Msafara wake leo Juni 06, 2024 katika Jimbo la Vunjo eneo la Himo mkoani Kilimanjaro na Kusikiliza Kero mbalimbali za Wananchi wa eneo hilo.
Msafara wa Katibu mkuu Dkt Nchimbi utahitimisha ziara ya mkoa wa Kilimanjaro leo kwa Kufanya mkutano mkubwa wa hadhara Wilayani Same kabla ya kuelekea Tanga kesho.
Dkt Nchimbi ameongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Rabia Hamid Abdallah pamoja na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Gavu.

Leave a Comment