×

Wananchi Wazidi Kunufaishwa na Zigo La Euro na Hisense Ya Tigo

Mshindi wa tiketi wapili kushoto akipokea mfano wa tiketi yake kwenye hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao.

Dar es Salaam 7 Juni 2024: Wanachi wazidi kuneemeshwa wamezidi kuneemeshwa na Kampeni ya Zigo la Euro na Hisense inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo kufuatia washindi  sita wa droo ya pili ya kampeni hiyo kukabidhiwa zawadi zao baada ya kuibuka kidedea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi hizo washindi, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta, amesema kuwa droo ya pili imeshafanyika na washindi sita walipatikana na hafla hiyo ilikuwa ni kwaajili ya kuwakabidhi zawadi zao.
Mary amesema droo hiyo imefanyika wiki ya pili na kuwapata washindi waliojishindia zawadi ya tiketi ya kwenda kushuhudia michuano ya Euro nchini Ujerumani, fedha taslim, televisheni na friji.
Kwa upande wa mshindi wa tiketi ya kwenda kushuhudia fainali za Euro, Emmanuel Mlonjela, amesema amefurahia sana  kupata bahati hiyo kwani ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu lakini sasa ilikuwa ndiyo imetimia na kuchukua nafasi hiyo kuwasihi watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Tigo kwa ajili ya huduma mbalimbali ikiwemo kufanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa, kununua muda wa maongezi, kulipa bili, malipo ya serikali na nyinginezo ili nao waingie kwenye droo ya kushinda zawadi hizo.

Leave a Comment