Travis Scott
Mwanamuziki Robin Rihanna Fenty, amekuwa akitoka kimapenzi na Mwanamuziki Jacques Webster ‘Travis Scott’ takriban mwaka mmoja sasa lakini jamaa huyo kwa usaliti anatisha.
Rihanna
Usaliti wa Travis umeonekana juzikati baada ya kunaswa akiwa na mwanamke mwingine wakiondoka kwenye klabu moja ya usiku iitwayo Hyde.
Paparazi wa mtandao mmoja unaodili na habari za mastaa aliwafuatilia Travis na mchepuko wake kishakuwapiga picha wakiwa kimahaba.
Kufuatia usaliti huo, mashabiki wa Rihanna wamemshauri kuangalia mwanaume mwingine wa kuwa naye ambaye siyo mwanamuziki kwani kila anayempa nafasi kwenye moyo wake anamtenda.