Kiungo wa kazi ngumu Saido Ntibanzokinza aliyefunga mabao 11 amepewa mkono wa asante ndani ya timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake msimu wa 2023/24.
Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza namna hii: “Uongozi wa klabu unautangazia umma kuwa hatutaendelea kuwa na mchezaji wetu Saido Ntibazonkiza baada ya mkataba wake kumalizika.”
Nyota huyo alikuwa kwenye ubora ndani ya kikosi cha Simba alikuwa namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu kwa mapigo huru upande wa penalti ambapo alifunga jumla ya mabao 7.
Katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi nyota huyo alifunga mabao mawili a timu hiyo iligotea hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikumbukwe kwamba John Bocco alikuwa mchezaji wa kwanza Juni 17 kutangazwa kuwa hatakuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2024/25.