×

Rais Samia Kushiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule, Cyril Ramaphosa Afrika Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum kuhusu Kutathmini hali ya Utendaji na Uchumi kwenye Vyombo vya Habari Tanzania Bara kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwandishi Mbobevu Tido Mhando wakati wa Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kuelekea Jamhuri ya Afrika Kusini leo jioni kwa ziara ya kikazi ya siku moja kushiriki hafla ya uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.

Rais Mteule Matamela Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuapishwa tarehe 19 Juni, 2024.

Leave a Comment