×

Ndugu wa Wanaodaiwa Kujiuza Sinza Wajitokeza Viunga Vya Mahakama Kudai Ndugu zao

Mmoja wa wanandugu wa waliokamatwa katika maeneo ya sinza jijini Dar es Salaam wakidaiwa kujiuza akizungumza jambo na waandishi wa habari.
Wakili Jebra Kambole (kulia) akiwa na baadhi ya ndugu hao nje ya viunga vya mahakama.

Watuhumiwa Wanaodaiwa kukamatwa katika maeneo ya Sinza siku kadhaa zilizopita wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza miili yao wamefikishwa jana Juni 19,2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine drive jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusomewa mashtaka yao yanayowakabili.

Licha ya kufikishwa katika mahakama hiyo lakini hawakusomewa mashtaka yao yanayowakabili na baadaye kurudishwa mahabusu tena ya polisi ambapo ndugu wa wadaiwa hao walionekana kujawa na hasira za kutaka kuachiwa kwa madai ya kuwa wengine wapo na watoto wachanga.

 

Leave a Comment