×

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina Afungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge – Video

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina, amefungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Juni 24, 2024 kwa kosa la kukiuka Kanuni za Bunge, kudharau Mamlaka ya Spika na mwenendo wa shughuli za Bunge, atarejea Bungeni katika kikao cha pili cha Novemba, 2024

Mpina ametiwa hatiani baada ya kuzungumza na Wanahabari kuhusu ushahidi aliouwasilisha kwa Spika kabla ushahidi huo haujawasilishwa mezani au kupewa idhini na Bunge kufanya hivyo

Awali, Mpina alidai Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alilidanganya Bunge kuhusu Uagizaji wa sukari Nchini

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema Mpina hatakiwi kufika eneo la Bunge wala kujihusisha na shughuli zozote za Bunge wakati wa adhabu yake

Leave a Comment