Mashabiki wa soka waliojishindia kwenye Kampeni ya ‘Zigo la Euro’ inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Ujerumani kushuhudia laivu michuano ya fainali za Ulaya ‘Euro 2024’ zinazoendelea nchini Ujerumani.
Washindi hao walipata nafasi hiyo kwa kutumia App mpya ya Tigo ya Super App na kubeti kwa kutumia kampuni ya Pari Match kwani nafasi na kujishindia safari za kwenda kushuhudia laivu fainali hizo bado zipo wanachotakiwa watumiaji wa simu kutumia mtandao wa Tigo na kupakua App mpya ya Tigo ya Super App pamoja na kubeti kwa kutumia kampuni ya Pari Match.