Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limetoa taarifa ya tukio la ajali iliyohusisha pikipiki (bodaboda) na gari aina ya Faw mali ya Kampuni ya TRANSAFRICA iliyosababisha vifo vya watu wanne akiwemo Dereva wa pikipiki hiyo na abiria watatu akiwemo Mtoto mwenye umri wa
miaka mitano ambao wote ni Wanafunzi kutoka Shule ya msingi Ipogolo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Alfred A. Mbena amesema “June 28,2024 usiku eneo la Mlima Ipogolo, Kata ya Kitanzini, Mkoani Iringa katika barabara Kuu ya Iringa – Dodoma, pikipiki ambayo ilitoroshwa mara baada ya ajali kutokea ikiendeshwa na Hassan Buruhani (17) Mkazi wa lpogoro akiwa amebeba abiria watatu, Helena Thomas (12) Wanafunzi wa darasa la saba, Ally Tenywa (09) Mwanafunzi wa darasa la kwanza na Gabriel Gongo (05) Mwanafunzi wa awali wote kutoka Shule ya msingi Ipogolo, iligonga ubavuni
upande wa kushoto wa gari namba RAG450N/RL 5167 aina ya FAW mali ya kampuni ya TRANSAFRICA ikitokea mkoani Ruvuma kuelekea Dodoma ikiendeshwa na Said Rashid (27) Mkazi wa Dar es salaam na kusababisha vifo kwa Dereva wa pikipiki na abiria wote watatu”
“Kutokana na chunguzi, tumebaini kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa pikipiki kujaribu kulipita gari hilo upande wa kushoto na kugonga ubavuni, kuanguka na kisha kukanyagwa na gurudumu za nyuma za gari hiyo”