
Kijana Hassan Michael mkazi wa Nungwi visiwani Unguja, ambaye ana kipaji cha kuwaigizia wanyama mbaliumbali wanavyotembea ikiwemo sokwe, amesema licha ya kuwa Watanzania wengi hawamfahamu, kipaji hicho kimempa fursa ya kusafiri nchi mbalimbali duniani.
Akizungumza na Global TV, Hassan alisema kuwa hapa nchini Tanzania hakuna anayemfahamu wala kujua kama ana kipaji kikubwa lakini ukweli ni kwamba anajulikana sana nje ya nchi na watu wengi wanatoka nje ya nchi kuja kumuona.